
Klabu ya Crystal Palace imemfuta kazi mkufunzi Patrick Vieira kama kocha mkuu klabuni hapo kufuatia mwenendo mbaya wa klabu hiyo iliyopokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Brighton siku ya Jumatano.
Palace ambayo ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi kuu England alama tatu tu juu ya mstari mwekundu imeshindwa kupata ushindi wowote kwenye mechi 12 mfululizo mpaka sasa mwaka huu.