
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu amesema Serikali ina mpango wa kuongeza hadhi ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kwa kuifanya taasisi hiyo iingiliane na Kiwanda cha Muziki na Filamu hapa nchini ili Watu wote wanaofanya shughuli za Utamaduni na Sanaa waone fahari ya kupita katika Chuo hicho.
Naibu Waziri Hamis Mwinjuma ameyasema hayo alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo.