
Baada ya kutafutwa kwa muda mrefu, hatimaye mwili wa mchezaji Christian Atsu umepatikana.
Wakala wa mchezaji huyo, Murat Uzunmehmet, amethibitisha kifo cha nyota huyo wa zamani wa Porto, Chelsea, Malaga na Newcastle.
“Mwili wa Atsu ulipatikana chini ya vifusi,” Uzunmehmet aliongeza wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Hatay, ambapo mwili wa mchezaji huyo ulipatikana. “Kwa sasa, vitu zaidi bado vinatolewa. Simu yake pia ilipatikana.”