
Msanii wa Nigeria, Burna boy ametangazwa kuwa ndiye atakayetumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi kwenye mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UCL) itakayofanyika Juni 10,2023 Istanbul nchini Uturuki. Mkurugenzi wa masoko wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Guy-Laurent Esptein amethibitisha.
Msimu uliopita mwanamuziki Camila Cabello ndiye aliyefanya show, ambayo hufanyika dakika 10 kabla ya mchezo huo wa fainali kuanza.