
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa maelekezo katika wiki ya nenda kwa usalama barabarani ikiwemo kulitaka Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, kuhakikisha mchakato wa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria na kanuni za usalama barabarani unafanyika kwa haraka, ili kuwa na sheria bora.
Maelekezo hayo, ameyatoa katika uzinduzi wa Wiki hiyo ya usalama barabarani Machi 15, 2023 na kuongeza kuwa, Baraza pia lifuatilie mfumo wa alama kwenye barabara na kwenye leseni za udereva, ili kuwabaini madereva wanaokiuka sheria na kuwachukulia hatua.