fbpx

Baraza la Umoja wa mataifa lawataka Urusi kuondoka Ukraine

Baraza kuu la Umoja wa mataifa limetoa wito wa kusitishwa vita nchini Ukraine na kuwataka Urusi kuondoka mara moja nchini humo, kwa kuzingatia mkataba wa Umoja wa mataifa.

Saa chache kabla ya mzozo huo kati ya Urusi na Ukraine kuingia katika mwaka wake wa pili, kupitia kikao chake maalumu cha dharura cha kumi na moja, baraza kuu limepitisha azimio jipya la usitishaji wa vita.

Matokeo ya kura zilizopigwa baada ya hotuba za wawakilishi wa mataifa wanachama wa umoja wa mataifa walioanza kuhutubia tangu jumatano, ni wanachama 141 ambao wameunga mkono huku wanachama 7 wakipinga.

Wanachama waliopinga azimio hilo la kumaliza vita Ukraine ni Belarus, jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, Eritrea, Mali, Nicaragua, Russiai na Syria. Nchi 32 zimejiweka pembeni yaani hazikuwa na upande wowote na miongoni mwazo ni China, india, Pakistan, Iran na Afrika Kusini.

Akihutubia kikao hicho, balozi wa Iran katika umoja wa mataifa, Saeed Iravani alisema pande zote zinazohusika katika vita vya Ukraine zinapaswa kuachana na malengo ya kijeshi na kutanguliza suluhu la kidiplomasia ili kufikia amani endelevu.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights