
Mfanyabiashara, Medrad Mbigi katika Mtaa wa Mpechi Halmashauri ya Mji wa Njombe anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Njombe kwa tuhuma za kumbaka mara kadhaa Mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka nane huku sababu ikitajwa kuwa ni imani za kishirikina.
RPC wa Njombe Hamis Issah amesema wanaendelea kufuatilia ili kubaini ulikoanzia ushirikina na kumkamata aliyesababisha jambo hilo.
Kamanda Issah ametoa wito kwa Wananchi wa Njombe kuwa makini na Watoto wao na kutoa taarifa mapema wanapoona vitendo vya ukatili kwa Watoto wao ili kudhibiti vitendo hivyo.