
Jeshi la Polisi mkoani Manyara limemtia mbaroni Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture, Joel Mollel maarufu Saitoti na wenzake 21 kwa tuhuma za kuongoza genge la Wachimbaji wadogo wadogo (Wana Apollo) na kuvamia mgodi wa madini ya Tanzanite uliopo Kitalu C katika Mji wa Mirerani wilayani Simanjiro.
Mgodi wa Kitalu C unaochimbwa kwa ubia kati ya Serikali na mwekezaji mzawa Onesmo Mbise ulivamiwa Marchi 12 mwaka huu majira ya kati ya saa 6.30 na saa 8 mchana na kundi hilo wakiwa na silaha za jadi na majabali makubwa yenye ncha kali na kufanikiwa kuwajeruhi zaidi ya wafanyakazi 10 wa kampuni ya Franone.