
Mkazi wa mtaa wa Mpechi, mkoani Njombe, Menrad Mbigi, mwenye umri wa miaka 28, anashikiliwa na jeshi la polisi, mkoani humo, kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kike wa kufikia mwenye umri wa miaka 8, tukio ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.
Kamanda wa polisi mkoani Njombe, Hamis Issa, amesema kuwa , uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea.