fbpx

Aliyemuua mwalimu mwenzake Geita kufanyiwa uchunguzi

Kamanda wa polisi Geita, Safia Jongo

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amesema mwalimu wa shule ya msingi Igaka mkoani Geita, Samweli Subi aliyemuua mwalimu mwenzake akiwa darasani kwa kumchoma kisu katika chembe cha moyo Emmanuel Chacha anafanyiwa uchunguzi zaidi kutokana tukio hilo alilolitenda.

Sababu ya Mwalimu Emmanuel Chacha (35) kuuawa na mwenzake imetajwa kuwa ni ugomvi wa madaraka ya uongozi katika kitengo cha elimu ya kujitegemea ambapo Kamanda Jongo amesema uchuguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights