
Sheldon Thomas, 35 ameachiwa huru akiwa ametumikia kifungo cha miaka 18 gerezani iliyoshababishwa na kitambulisho cha picha ya udanganyifu.
Mwanaume huyo alipatikana na hatia ya mauaji kupitia shahidi aliyemtambua mtu tofauti mwenye jina moja anayeishi katika eneo moja.
“Asante, mheshimiwa, kwa kuruhusu hili kutokea,” Thomas alisema. “Nimesubiri kwa muda mrefu.”
Thomas alisema anamsamehe mpelelezi wa NYPD, mashahidi na wengine waliohusika katika mashtaka yake na kufungwa kwa mauaji ya Anderson Bercy mwenye umri wa miaka 14, ambaye muuaji wake wa kweli bado hajajulikana.