
Mkazi wa kijiji cha Kiperesa wilayani Kiteto mkoani Manyara mwanaume mmoja aitwae Issa Shabani mwenye umri wa miaka 32 amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na Tembo walioonekana kijijini hapo wakati alipojaribu kupiga picha ya selfie na Tembo hao.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara, RPC George Katabazi amesema tukio hilo limetokea machi 12/2023 ambapo Tembo watatu walionekana wakiwa kwenye mashamba yaliyopo karibu na makazi ya watu wa kijiji cha Kiperesa.