
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kukutwa na meno sita ya Tembo wilayani Same.
Kamanda wa polisi mkoani kilimanjaro Simon Maigwa, amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni kutokana na operesheni zinazoendelea za kukabiliana na matukio ya uhalifu katika mkoa huo.