
Mahakama ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, imemhukumu Mohamed Ngwerekwe (25) mkazi wa Kijiji cha Namiungo kwa kosa la kumnajisi mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka minne.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Honorius Kando ambaye alisema, mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti katika kijiji hicho.
Alisema mtuhumiwa ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 158 kifungu kidogo cha(1)(a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019.
Hata hivyo, mtuhumiwa wakati akisomewa maelezo ya awali, alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba Mahakama impunguzie adhabu.