
Rapa Kanye West amedaiwa kufikia makubaliano na kampuni ya Adidas katika kuuza bidhaa za Yeezy zilizobaki ambazo Adidas walishindwa kuziuza bila Kanye West.
Endapo ni rasmi wamefikia makubaliano basi kampuni ya Adidas watakuwa wameokoa zaidi ya Tsh.trilioni 1.3 ambazo walibidi wazipoteze kwa mwaka huu 2023.
Lakini hata hivyo haijulikana kama wataendelea kushirikiana kibiashara baada ya bidhaa hizo kumalizika sokoni. Kumbuka Oktoba mwaka jana 2022 kampuni hii ilimtema kanye huku wakisahau kwamba walizalisha bidhaa lukuki zenye chapa ya Yeezy.
Hivyo kushindwa kuziuza na kuzikalia ndani tu, ikiwa kisheria hairuhusiwi kutumia brand jina la mtu katika biashara yako kama hamjakubaliana au hamjaingia Katika mkataba.