fbpx

Adaiwa kuuawa na mpenzi wake kisha kuchomwa moto

Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Josephine Mngara (27), mkazi wa Mtemboni, mji mdogo wa Himo, mkoani Kilimanjaro anadaiwa kuuawa na mpenzi wake na kisha mwili wake kuchomwa moto.

Mwili huyo umekutwa kwenye pagale ukiwa umechomwa na kuteketea kwa moto ambapo mabaki ya mwili huo yamehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya kanda ya kaskazini (KCMC).

Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa wilaya ya moshi, Kisare Makori amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kwenye nyumba aliyokuwa akiishi marehemu na mume wake imekutwa michirizi ya damu kuelekea eneo ambalo mabaki ya mwili huo yamekutwa. Amesema jeshi la polisi linaendela na uchunguzi wa tukio hilo.

Aidha amesema jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa kitaalamu ikiwemo kuchukua sampuli ya vinasaba (DNA) na kupeleka kwa mkemia mkuu wa serikali ili kujiridhisha na tukio hilo.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights